Mark 4:13-18

13Kisha Isa akawauliza, “Hamwelewi maana ya mfano huu? Basi mtaelewaje mifano mingine? 14 aYule mpanzi hupanda neno. 15 bHawa ndio wale walio kando ya njia ambako neno lilipandwa. Walisikiapo neno, Shetani huja mara na kulinyakua lile neno lililopandwa ndani yao. 16Nazo zile mbegu zilizoanguka kwenye udongo wenye miamba, ni wale wanaolisikia neno, na mara hulipokea kwa furaha. 17Lakini kwa kuwa hawana mizizi, wao hudumu kwa muda mfupi tu. Kisha dhiki au mateso yanapoinuka kwa ajili ya lile neno, mara wao huiacha imani. 18Lakini wengine, kama mbegu iliyopandwa kwenye miiba, hulisikia lile neno;
Copyright information for SwhKC